Marekani yaendeleza msaada kwa Ukraine

Ikiwa imebaki miezi miwili utawala wa Rais Joe Biden, umalizike, Marekani inazidisha msaada wa kifedha, kijeshi na kidiplomasia kwa juhudi za Kyiv, kujilinda dhidi ya uvamizi wa Russia.

Katika mkutano wa G20, Rio de Janeiro, Brazil, ambapo viongozi wa mataifa 20 makubwa kiuchumi duniani wanakutana, maafisa wa Marekani wanashinikiza uwezekano wa kuwepo kwa lugha ya nguvu zaidi kuhusu Ukraine, Naibu Mshauri wa Usalama wa Kitaifa, John Finer ameiambia VOA wakati wa mkutano wa Jumatatu.

Wanadiplomasia wa nchi za Magharibi wamesisitiza tena msukumo wa Moscow kukosolewa vikali kwa shambulizi lake la anga mwishoni mwa juma, likiwa ni kubwa zaidi katika eneo la Ukraine katika miezi kadhaa iliyopita.

Pia wameonya juu ya kuongezeka kwa juhudi za vita vya Russia, ambavyo vinaweza kuwa na athari ya kudhoofisha zaidi bara la Ulaya.