Marekani yaanza kutoa mafunzo dhidi ya ugaidi yanayofanyika kila mwaka

Sherehe za ufunguzi wa mafunzo yanayojulikana kama Flintlock yanayo endeshwa na Marekani katika chuo cha mafunzo ya kijeshi Jacqueville, Ivory Coast, Feb. 20, 2022.

Program ya mafunzo ya kila mwaka kwa ajili ya kupambana na ugaidi yanayotolewa na Marekani yameanza Jumapili nchini Ivory Coast.

Wakati mafunzo haya yakiendelea waasi wa Kiislamu wenye msimamo mkali wanadhibiti sehemu kubwa, mapinduzi yakiwa juu, na vikosi vya Ufaransa vinajipanga kuondoka.

Mafunzo hayo yanayojulikana kama Flintlock yatawaweka pamoja zaidi ya wanajeshi 400 kutoka Afrika Magharibi kuinua taaluma za vikosi ambavyo vingine vinakabiliwa na mashambulizi ya makundi yenye silaha yanayojihusisha na al-Qaida na Islamic State.

Wale ambao hawatokuwepo ni pamoja na vikosi vya Guinea na nchi mbili ambazo zimepigwa vibaya na ghasia za Waislamu wenye msimamo mkali , Mali na Burkina Faso.

Wanajeshi wamenyakua madaraka katika nchi hizo tatu tangu mwaka 2020, hatua iliyozusha wasiwasi kuhusu kurejea tena mtazamo wa utawala wa kikoloni Afrika Magharibi, kama ukanda wa mapinduzi.