Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 21:29

Ufaransa na washirika wake kuwaondoa wanajeshi wao Mali


FILE - kikosi cha Ulaya nchini Mali, Jumatano Juni 9, 2021. (AP Photo/Jerome Delay, File)
FILE - kikosi cha Ulaya nchini Mali, Jumatano Juni 9, 2021. (AP Photo/Jerome Delay, File)

Ufaransa na washirika wake katika kikosi cha Ulaya nchini Mali wametangaza Alhamisi wanajeshi wake wataondolewa kutoka Mali baada ya miaka 10 ya kupambana na uasi unaoendeshwa na wapiganaji wa Kiislamu.

Taarifa iliyosainiwa na viongozi wa nchi za Sahel, Ufaransa na Ulaya inaeleza kwamba vizingiti mbali mbali vilivyowekwa na utawala wa kijeshi wa Mali vimesababisha hali kuwa ngumu kuweza kuendelea kufanya kazi nchini humo.

Uamuzi wa kuwaondoa wanajeshi wa kikosi cha Ufaransa cha Barakane na kile cha nchi za Ulaya Takuba ulichukuliwa mjini Paris kufuatia mkutano kati ya Rais Emmanuel Macon na viongozi wa nchi za Afrika Magharibi kutoka ukanda wa Sahel.

Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi akiwa pamoja na Marais Macky Sall, wa Senegal na Nana Akufo-Addo wa Ghana, ambaye pia ni mwenyekiti wa ECOWAS, Rais Macron amesema kutoheshimiwa kwa mazingira ya kisiasa na kisheria kumesababisha hali kuwa ngumu kufanya kazi za kijeshi kupambana na ugaidi nchini Mali.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wapili kulia, akimsikiliza Rais wa Ghana Nana Afuko Addo, kulia, akiwa na Rais wa Senegal Macky Sall, na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel, kushoto, wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu ya ushiriki wa Ufaransa katika eneo la Sahel.(Ian Langsdon, Pool via AP)
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wapili kulia, akimsikiliza Rais wa Ghana Nana Afuko Addo, kulia, akiwa na Rais wa Senegal Macky Sall, na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel, kushoto, wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu ya ushiriki wa Ufaransa katika eneo la Sahel.(Ian Langsdon, Pool via AP)

Rais wa Ufaransa anaeleza haya:“Ufaransa na washirika wake wanaohusika katika kazi ya kupambana na ugaidi, yaani mataifa yanayohusika kwenye kikosi cha Takuba yameamua kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Mali. Kufungwa kwa kambi zetu kutafanyika kwa ushirikiano na jeshi la Mali na kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali. Wakati huo wote tutaendelea kukisaidia kikosi cha Minusma.

Kabla ya kutoa tangazo hilo Rais Macron aliwaalika viongozi wa Senegal, Chad, Mauritania na Niger, bila ya kuwaalika viongozi wa Mali na Burkina Faso.

Rais wa Senegal Macky Sall, anasema wamefikia makubaliano kuziachia nchi za Sahel jukumu la kupambana na ugaidi pekee yao.

Rais wa Senegal ameeleza haya: "Tumekubaliana na wenzetu wa Ulaya kwamba vita dhidi ya ugaidi katika Sahel vitakua ni jukumu pekee la nchi za Afrika. Jambo hilo limefikiwa kwa maridhiano na tnafurahi kwamba makubaliano mepya yamefikiwa kwa wanajeshi hao kubaki katika kanda hiyo na majukumu yao kupangwa upya.”

Wakazi wa mji mkuu wa Bamako wamekuwa na maoni yanayo tofautiana kuhusu uamuzi huo kuna baadhi waliofurahia kama Zoumana Doakite.

Zoumana Diakite, Mkazi wa Bamako amesema: "Barkhane ni kikosi ambacho kimekuwepo hapa kwa miaka 9 bila ya matokeo yeyote, kinyume chake tunasikitishwa na vifo vinavyotokea kila siku. Ikiwa kuondolewa kwao kutafikisha kikomo vita hapa Mali, basi liwalo na liwe.”

Kuna wakazi wengine wanaosema inabidi kuchukua tahadhari kutokana na matokeo yake uamuzi huo. Lassana Traore anasema huwezi kuchukua uwamuzi wa ghafla bila ya kutafakari vyema

Lanssana Traore, Mkazi wa Bamako anaeleza: “Tumekua washirika kwa miaka mingi. Sisi ni washirika. Hatuweza kufanya kitu bila ya Ufaransa, na Ufaransa haiwezi kufanya kitu bila sisi. Kwa hivyo tusiwatupe kama tunavyotupa takataka. Na ufaransa pia isitudharau.

Mivutano kati ya Mali na Ufaransa ilijitokeza hasa baada ya baraza la kijeshi lililofanya mapinduzi ya pili mwaka jana na kukiuka makubaliano ya kuitisha uchaguzi baada ya miezi 18.

mbali na suala hilo nchi za Magharibi zinaituhumu Mali kwa kuwatumia karibu Mamluki 800 kutoka kampuni ya Rashia ya Wagner.

Uamuzi unahusu kuondolewa vikozi viwili, kile cha ufaransa Barakane, chenye wanajeshi 2 400 ambao hivi sasa watahamishwa hadi nchi jirani ya Burkina Faso na kikosi cha Takuba cha mamia kadhaa ya wanajeshi wa nchi za ulaya.

Wanajeshi wa kigeni wanoabaki Mali kwa hivi sasa ni wale wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha MINUSMA.

XS
SM
MD
LG