Msururu wa mashambulio ya masafa marefu ya Russia yalilenga miundombinu ya Ukraine yamekuwa yakitokea wakati Rais wa Russia Vladmir Puttin akihitimisha mikutano na makamanda wake wa jeshi kutafuta mapendekezo ya jinsi wanavyofikiri uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine unapaswa kusonga mbele , Kremlin imesema.
Wizara ya ulinzi ya uingereza imesema taarifa za kijasusi za leo katika siku za karibuni, zimeeleza kuwa kumekuwa na kampeni za Russia za kufanya mashambulizi ya masafa marefu dhidi ya miundombinu muhimu ya Ukraine.
Wizara hiyo iliandika katika mtandao wa Tweet, “ wimbi la mashambulizi limelenga zaidi makombora ya anga na baharini lakini kwa hakika yamejumuisha pia usafiri uliotolewa na Iran- UAVs, kurusha makombora kutoka mkoa wa Krasnodar huko Russia.
Mratibu wa baraza la usalama la taifa kwa ajili ya mkakati wa mawasiliano John Kirby ameiambia sauti ya Amerika katika mahojiano siku ya Ijumaa kwamba Marekani itatoa msaada zaidi wa usalama kwa ajili ya Ukraine.
Alipoulizwa kama Washington itatii onyo la Russia la kutowasilisha makombora ya kisasa ya ulinzi wa anga au kukumbwa na hatari , Kirby alijibu kwa kusema “ Russia haiwezi kuamuru Marekani au nchi yoyote katika msaada wa usalama inaotoa kwa Ukraine.”