Marekani imesema Alhamisi kuwa wao na wanachama wengine wa G7 wataipatia Kyiv mkopo wa hadi dola bilioni 50 ambao zitalipwa kwa washirika wa Magharibi kwa kutumia mapato ya riba kutoka kwenye mali za Russia zilizozuiliwa katika taasisi za kifedha za Magharibi.
Tangazo hilo lilikuja wakati Rais Joe Biden akikutana na viongozi wa Kundi la nchi saba tajiri za demokrasia Alhamisi katika hoteli ya kifahari ya Borgo Egnazia huko Puglia, Italia, katika siku ya kwanza ya mkutano huo.
Biden amekuwa akiwashinikiza viongozi wa G7 kukubaliana na mpango wake kwa washirika wa Magharibi kutoa fedha mapema kwa Ukraine na kulipwa kwa kutumia mapato ya riba kutoka dola bilioni 280 za mali zisizohamishika za Russia.