Marekani na Uturuki zazungumzia masuala ya NATO na Ukraine

Marekani na Uturuki, Jumatano ziliweka pembeni tofauti ambazo zimezorotesha uhusiano wao kwa miaka mingi.

Licha ya hayo hazikuweza kuripoti maendeleo katika kutatua mizozo kuhusu uvamizi wa Russia, kwa Ukraine, na upanuzi wa NATO ambao umeharibu uhusiano kati ya washirika.

Katika mkutano uliofanyika Washington, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu, walikuwa na nia ya kufikia utatuzi huo, lakini hakukuwa na dalili ya mara moja ya maafikiano, ingawa wote wawili walipongeza ushirikiano kati ya nchi zao.

Wakipongeza ushirikiano juu ya Ukraine, na Blinken alisifu uongozi wa Uturuki katika kufanikisha mpango wa usafirishaji wa nafaka za Ukraine.

Lakini katika maelezo mafupi kabla ya mkutano wao, hakuna hata mmoja aliyetaja tofauti zao juu ya kujiunga kwa Finland na Sweden katika NATO, ambayo Waturuki wamezuia hadi sasa licha ya kuungwa mkono kwa nguvu na Marekani na washirika wengine.