Marekani na Ufaransa kuimarisha uhusiano

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken akishuka kwenye ndege alipowasili Ufaransa.Oktoba 4,2021.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani  Antony Blinken yuko Paris kwa mikutano na maafisa wa Ufaransa kujaribu kuboresha uhusiano kati ya washirika hao

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken yuko Paris kwa mikutano na maafisa wa Ufaransa kujaribu kuboresha uhusiano kati ya washirika hao wawili kufuatia mzozo kuhusu ushirikiano wa usalama kati ya Marekani, Uingereza na Australia.

Blinken aliianza Jumanne kwa kukutana na Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian, na alipoulizwa ni vipi atahakikisha Ufaransa inaweza kuamini Marekani, Blinken aliwaambia waandishi wa habari, "Tutakuwa na nafasi ya kuzungumza baadaye."

Ratiba yake pia ilijumuisha mazungumzo na mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Ufaransa Emmanuel Bonne na kuongoza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo na Waziri Blinken pia atakutana na wenzake wa Ufaransa kuendelea na majadiliano juu ya kuimarisha zaidi uhusiano muhimu wa Marekani na Ufaransa juu ya maswala mbali mbali ikiwa ni pamoja na usalama katika eneo la Indo-Pacific, mzozo wa hali ya hewa, kufufua uchumi kutokana na janga la COVID-19, uhusiano wa transatlantic , na kufanya kazi na washirika wetu katika kushughulikia changamoto na fursa za ulimwengu, ilieleza wizara ya mambo ya nje ilieleza katika taarifa yao ya Ijumaa.