Marekani na washirika wake 11, Jumatano kwa pamoja waliwaonya wanamgambo wa Kihouthi wa Yemen, kuhusu madhara ambayo hayajabainishwa na kuwataka wasitishe mashambulizi dhidi ya meli zinazosafiri kupitia bahari ya Sham.
“Waache ujumbe wetu sasa uwe wazi, na tunatoa wito wa kukomeshwa mara moja kwa mashambulizi haya haramu na kuachiliwa kwa meli na mabaharia wanaozuiliwa kinyume cha sheria,” nchi hizo zilieleza katika taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani.
Imeendelea kueleza kwamba Wahouthi watabeba jukumu la maafa iwapo wataendelea kutishia maisha, uchumi wa dunia na mwendendo wa biashara katika njia muhimu za maji za ukanda huo,nchi hizo 12 zimesema.
Zilizotia saini kwenye taarifa hiyo ni pamoja na Uingereza, ambayo Jumatatu ilitoa onyo lake kwa Wahouthi, pamoja na Australia, Canada, Ujerumani na Japan.