Marekani inasema inajiondoa kutoka shirika la elimu na sayansi la Umoja wa Mataifa- UNESCO ikiishutumu taasisi hiyo kwa uwonevu dhidi ya Israel. Wizara ya mambo ya nje Marekani ilithibitisha kwamba Marekani itajiondowa rasmi Disemba 31 mwaka 2018.
Saa kadhaa baadae Israel ilitangaza kwamba pia itajitoa kutoka uanachama wa taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa-UNESCO. Taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ilisema Waziri Mkuu aliielekeza wizara ya mambo ya nje kuandaa barua ya Israel kujitoa kutoka taasisi hiyo ikiungana na Marekani.
Bwana Netanyahu aliukaribisha uamuzi uliofanywa na Rais wa Marekani Donald Trump wa kujitoa kutoka UNESCO. Kwa upande wake UNESCO ilijibu kwa masikitiko uamuzi huo uliofanywa na Marekani.