Waziri wa fedha wa Marekani, Janet Yellen, Jumapili amemwambia Waziri Mkuu wa China, Li Qiang, kuwa uwezekano wa kufanya mazungumzo magumu umeyaweka mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa sana kwenye msimamo thabiti zaidi katika kipindi cha mwaka uliopita.
Walipoanza mkutano mjini Beijing, Li alijibu kuwa nchi hizo mbili zinahitaji kuheshimiana na zinapaswa kuwa washirika, na si maadui, na kuongeza kuwa maendeleo yenye manufaa yamepatikana wakati wa ziara ya waziri Yellen.
Amesema waziri Yellen, kwamba Washington na Beijing zimekuwa na wajibu wa kusimamia kwa uwajibikaji uhusiano huo mgumu, alipokuwa akiwasilisha hoja yake ya kudhibiti uwezo wa ziada wa viwanda wa China kwa uongozi wa China.
Alielezea pia wasiwasi wake kuhusu uwezo uliopitiliza wa kiviwanda wa China na athari kwa wafanyakazi wa Marekani, kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya fedha.