Mkufunzi huyo wa matumizi ya bunduki ambaye alikulia katika eneo hilo, alipatikana amekufa katika eneo la Lisbon, Gavana Janet Mills alisema katika mkutano wa wanahabari Ijumaa usiku.
Card anashukiwa kutekeleza mauaji hayo katika ukumbi wa kucheza mpira wa Bowling na pia kwenye baa moja mjini Lewiston siku ya Jumatano.
Baada ya mashamulizi hayo, wakazi wa Maine waliokumbwa na wasiwasi na hofu walisalia nyumbani mwao kwa siku mbili mfululizo huku Card akitafutwa na maafisa wa usalama.
April Stevens, mkazi wa Lewiston ambaye alimfahamu mmoja wa waathiriwa, alisema alifarijika kujua kwamba "mnyama na mwoga" ambaye alisababisha maumivu mengi hakuwa tishio tena.
"Nimefarijika lakini sina furaha," alisema. "Kulikuwa na vifo vingi sana. Watu wengi sana waliumia. Hali imetulia...ndiyo, lakini furaha...hapana."
Kamishna wa Idara ya Usalama wa Umma wa Maine Mike Sauschuck alisema mwili wa Card ulipatikana saa moja na dakika 45 jioni karibu na Mto Androscoggin, umbali wa takriban kilomita 13 kusini-mashariki mwa pahali ambapo ufyatuaji risasi wa pili ulitokea Jumatano jioni.
Alikataa kufichua eneo hilo lakini afisa mmoja aliambia The Associated Press mwili huo ulikuwa kwenye kituo cha kuchakata tena ambapo Card alikuwa imefukuzwa kazi katika siku za nyuma.
Mapema Ijumaa mkuu wa polisi katika jimbo la Maine Kanali William Ross alikuwa amesema mshukiwa Card, alipaswa kuchukuliwa kuwa mtu mwenye silaha na hatari” na kwamba watu ambao wangekutana naye walipaswa kuwaita polisi badala ya kukabiliana naye.
Polisi na maafisa wengine wa usalama Alhamisi walionekana kwa wingi kwenye nyumba iliyoko Lewiston ya ndugu wa Card.
Shule za umma za Lewiston na shule za wilaya karibu na Lewiston zilifungwa Ijumaa wakati mamlaka zikiendelea na msako wao.