Marekani kuondoka WHO?

Rais mteule wa Marekani Donald Trump. Dec 22, 2024

Wanachama wa kamati ya maandalizi ya utawala wa rais mteule wa Marekani Donald Trump, wanapanga mikakati ya kuiondoa Marekani kutoka kwa shirika la afya duniani WHO, punde baada ya kuapishwa kwa Trump.

Jarida la Financial times, limeandika ripoti hizo kwa kunukuu wataalam wawili wenye taarifa za uhakika na mpango huo.

Mtaalam wa pili ni Ashish Jha, aliyekuwa kwenye kamati ya white house ya kupambana na janga la virusi vya Corona.

Timu ya maandalizi ya utawala wa Trump haikujibu ombi la kutaka kuzungumzia ripoti hiyo.

Mpango wa kuondoa Marekani kutoka shirika la afya dunia unaendana na ukosoaji wa muda mrefu wa Trump kuhusu kazi za shirika hilo..