Marekani ilijindoa kwenye shirika hilo mwezi Disemba mwaka wa 2018 chini ya utawala wa Rais Donald Trump kwa madai kuwa UNESCO inachukua hatua za kuegemea dhidi ya Israel na usimamizi wake ni mbaya.
“Ni kitendo cha imani ya dhati kwa UNESCO na ushirikiano wa kimataifa,” mkurugenzi mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay amesema katika taarifa akitangaza Marekani kujiunga tena na shirika hilo.
Mpango uliopendekezwa lazima uwasilishwe kwa kongamano kuu la nchi wanachama wa UNESCO ili kuidhinishwa, na baadhi ya nchi wanachama zimeitisha kikao maalum kitakachofanyika siku za usoni ili kuchukua maamuzi.
Marekani inachangia asilimia 25 ya fedha kwenye shirika hilo lenya makao yake mjini Paris.