Kutambuliwa huko kunazipa nchi ambazo sio wanachama wa muungano wa NATO kunufaika na misaada ya kijeshi na fedha kama nchi wanachama wa NATO, lakini bila makubaliano ya pande zote kuhusu ulinzi ambayo yanaunganisha nchi wanachama wa NATO.
Afisa mkuu wa utawala wa Biden aliwaambia waandishi wa habari Jumatano kwamba Biden atalitaarifu Bunge la Marekani kuhusu utambuzi huo, ambako unachukua siku 30 kabla ya kuanza kutekelezwa.
Afisa huyo alisema hatua hiyo inalenga kuiinua Kenya na kukiri kweli kwamba Kenya ni mshirika wa Marekani kimataifa.
Wakati huo huo, Ruto na Biden watatumia majadiliano yao ya leo kutafuta suluhu ya mpango wa Kenya wa kutuma maafisa wa polisi 1,000 nchini Haiti.
Mpango huo ambao Marekani imeahidi kutoa ufadhili wa dola milioni 300, unakabiliwa na changamoto kubwa za kisiasa na kisheria nchini Kenya.