Marekani kuisaidia Taiwan

Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Marekani, Michael McCaul alisema Jumamosi kuwa Marekani itasaidia kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Taiwan na kuharakisha uwasilishaji wa silaha, wakati China ikianza siku tatu za mazoezi ya kijeshi kuzunguka kisiwa hicho kinachojitawala.

Akizungumza katika hafla ya chakula cha mchana mjini Taipei, McCaul alionyesha uungaji mkono wa Marekani kwa Taiwan. “Ninatia saini kwa utoaji huo na tunafanya kila tuwezalo kuharakisha hili,” alisema.

Amesema amani kupitia nguvu ni ya kweli, na ndiyo sababu tunahitaji kuifanya Taiwan kuwa na uwezo.

Njia moja ya kuharakisha upelekaji wa silaha nchini Taiwan, McCaul alisema, ni kutathmini maeneo hatarishi na yenye tishio kubwa na kupanga upya utaratibu wa uwasilishaji wa silaha.

Jeshi la China lilisema doria za utayari wa shughuli za kijeshi Jumamosi na mazoezi ya karibu na Taiwan yameanza kama ilivyopangwa, na kutoa onyo kwa vikosi vya kujitenga vya Taiwan na vikosi vya nje vyenye njama na uchochezi.