Shirika hilo limefafanua kuwa abiria wanaosafiri kwenye dazeni ya ndege za mashariki ya kati na Afrika ya kaskazini kuelekea Marekani watazuiwa kuingiza laptop na vifaa vingine vya kielektroniki ndani ya ndege ziendazo nchini humo..
Marufuku hiyo imetangazwa Jumatatu katika taarifa ya shirika la ndege la Royal Jordan na shirika la habari rasmi la Saudia Arabia. Inatarajiwa kuanza kutumika Jumanne.
Shirika la ndege la ufalme wa Jordan limesema katika mtandao wake wa Twitter kwamba abiria wanaokwenda Marekani watazuiwa kubeba vifaa vyao vingi vya kielektroniki ndani ya ndege kwa maagizo ya maafisa wa Marekani ikiwa ni pamoja na wale wanaopitia Canada.Tweet hiyo tangu wakati huo imefutwa.
Marufuku hayo hayajumuishi simu za mkononi au vifaa vya matibabu, lakini inajumuisha laptop michezo ya kielektronik, na kamera .Vifaa hivyo vinaweza kuwekwa kwenye eneo la kubeba mizigo mikubwa ya ndege.
Shirika la ndege la US Airline halitaathirika kwasababu haipiti katika nchi zote zilizotajwa kuzuiwa kuingia na laptop ndani ya ndege kuelekea Marekani.