Biden amesema “Tunabadili hali ilivyo hapa, kama tusemavyo kila mara, tuko katika hali isiyo ya kawaida katika historia, ambapo maamuzi tunayochukua leo yataongoza mwelekeo wa ulimwengu wetu kwa miongo kadhaa ijayo bila shaka.”
White House imebaini kuwa Marekani haswa inataka teknolojia isaidie kuimarisha demokrasia na sio kwa kupinga demokrasia.
Katika muktada huo, mawaziri wakuu wa nchi nane za Ulaya wamesaini barua na kuiwasilisa kwa wakuregenzi watendaji wa kampuni kubwa za mitandao ya kijamii wakiwataka kuchukua hatua madhubuti kwa kuzuia usambazaji wa habari za uongo kwenye mitandao yao.
Barua hiyo imesainiwa na viongozi wa Ukraine, Moldova, Poland, Jamhuri ya Czech, Estonia, Latvia, Lithuania na Slovakia.
Viongozi 120 wa dunia ndio walishiriki mkutano huo kwa njia ya mtandao.