Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema katika taarifa kwamba kikosi cha kijeshi cha RSF kinastahili kuacha kupiga makao ya raia na badala yake kuwalinda raia hao katika sehemu za Nyala, Omdurman na kote Sudan.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, wapiganaji wa RSF wamekuwa wakipigana na wanajeshi wa Sudan tangu mwezi Aprili katika vita ambavyo vimepelekea vifo vya zaidi ya watu 5000 na kupelekea zaidi ya watu milioni 5 kukoseshwa makazi.
Wapiganaji wa RSF wameongeza mashambulizi katika sehemu za Omdurman zinazoshikiliwa na wanajeshi wa serikali. Kundi hilo lia limeendelea kutekeleza mashambulizi kwenye kambi za kijeshi katika sehemu za Nyala, magharibi mwa Darfur, wakiwa na lengo la kuudhibithi mji huo.