Netanyahu alivunja baraza hilo Jumatatu, uamuzi ambao ulitarajiwa baada ya Jenerali wa zamani Benny Gantz, mwanasiasa wa mrengo wa kati kuondoka katika baraza hilo wiki iliyopita.
Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari katika White House, Kirby alisema kwamba Netanyahu alikuwa na haki ya kuchukua hatua hiyo, na kusisitiza kuwa Rais Joe Biden ataendelea kufanya kazi pamoja na Netanyahu licha ya kutokubaliana kwao katika masuala fulani.
Gantz alijiunga na serikali ya umoja ya Netanyahu mwezi Oktoba wakati vita vilipoanza na aliomba liundwe baraza la vita. Netanyahu amelivunja baraza hilo bila Gantz kuwepo.
Naye msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Matthew Miller aliwambia waandishi wa habari kwamba sio jukumu la Marekani kuamua nani anatakiwa kuwa katika serikali ya Israel.