Marekani inajibu kwa tahadhari kuhusu mazungumzo ya Iran na Saudia

Rais wa Marekani, Joe Biden

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran, Saeed Khatibzadeh alithibitisha mazungumzo na Riyadh katika mkutano wa waandishi wa habari hapo Jumatatu. Alisema kupunguza mivutano kati ya mataifa hayo mawili ya kiislam katika eneo la ghuba ya kiajemi ni kwa maslahi ya mataifa yote

Marekani imejibu kwa tahadhari uthibitisho kwamba hasimu wake wa mashariki ya kati, Iran amekuwa akifanya mazungumzo ya nadra na mshirika wa Marekani, Saudi Arabia juu ya kufufua uhusiano uliovunjika kati ya mataifa haya mawili Jirani yenye nguvu kieneo.

Katika taarifa ya Jumanne iliyotumwa kwenye idhaa ya kiajeni ya VOA, afisa mwandamizi wa utawala wa Biden alisema Marekani imeona ripoti za mazungumzo ya karibuni kati ya Tehran na Riyadh bila ya kutaja wapinzani hao wawili, ofisa huyo aliongeza; ni lengo la Marekani kupunguza mivutano katika eneo hilo na tunahisi kwamba pande zote zinapozungumza na kila mmoja ni hatua nzuri katika juhudi hizo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran, Saeed Khatibzadeh, alithibitisha mazungumzo na Riyadh katika mkutano wa waandishi wa habari hapo Jumatatu. Alisema kupunguza mivutano kati ya mataifa hayo mawili ya kiislam katika eneo la ghuba ya kiajemi, ni kwa maslahi ya mataifa yote na eneo.

Khatibzadeh aliongeza kuwa, tunakaribisha kutatua masuala ambayo yamejitokeza kati ya mataifa haya mawili, tutatumia juhudi zetu kadri tuwezavyo katika hili.

Matamshi rasmi ya kwanza ya Saudi Arabia juu ya mazungumzo haya yamekuja Mei 7, katika matamshi yaliyotolewa na ofisa wa wizara ya mambo ya nje wa Saudi Arabia, Rayed Krimly kwa shirika la habari la Reuters.