Marekani imetangaza vikwazo zaidi vya kiuchumi dhidi ya Russia

Vladimir Potanin, mfanyabiashara zaidi sana nchini Russia akizungumza wakati wa kongamano kuhusu uekezaji mjini Moscow, Russia, Sept 23, 2014.

Marekani imewekea Russia vikwazo vipya vya kiuchumi kwa kulenga mfanyabiashara tajiri sana nchini humo Vladimir Potanin na familia yake.

Hatua hiyo ni ya hivi punde, ya kuishinkiza Moscow kuachana na vita vyake nchini Ukraine.

Potanin, aliwahi kuwa naibu wa waziri mkuu wa Russia, na Marekani imesema kwamba ana uhusiano wa moja kwa moja na rais wa Russia Vladimir Putin.

Potanin, mwenye umri wa miaka 61, anasimamia kampuni ya uekezaji ya Interros yenye umihumu mkubwa kwa uchumi wa Russia, ikiwemo kumiliki asilimia 36 ya kampuni kubwa ya kutengeneza Nikel duniani, ya Norkickel.

Uingereza na Canada zilimwekea vikwazo vya kiuchumi Potatin.

Wizara ya fedha ya Marekani vile vile imewekea vikwazo benki ya biashara ya Russia ya Rosbank ambayo Potanin alipata haki za umiliki wake mapema mwaka huu pamoja matawi 17 ya benki ya VTB ambayo ndio benki kubwa zaidi nchini Russia.