Serikali ya Marekani imewawekea vikwazo maafisa watatu wa ngazi ya juu wa Korea kaskazini, wanaohusiana na mpango wa utengenezaji wa silaha za nyuklia, baada ya Pyongyang kufanya majaribio kadhaa ya makombora yake ya masafa marefu.
Wizara ya fedha ya Marekani imetaja watu hao kuwa Jon il Ho, Yu Jin, na Kim Su Gil ambao vile vile waliwekewa vikwazo na umoja wa ulaya mnamo mwezi April.
Vikwazo vya hivi punde vya Marekani vimetangazwa baada ya Korea kaskazini kufanya majaribio ya zaidi ya makombora 60 mwaka huu, huku kukiwepo wasiwasi kwamba huenda nchini hiyo inakaribia kuanza tena majaribio ya silaha za nyuklia, ambayo haijafanya tangu mwaka 2017.
Marekani imesema kwamba Jon Il Ho na Yu Jin, ametekeleza majukumu makubwa katika utengenezaji wa silaha za uharibifu mkubwa, kutokana na nafasi yake kama mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza silaha cha Korea kaskazini.