Marekani imetangaza sera ya kuzuia Visa kwa watu binafsi nchini Ghana

Mfano wa Visa ya Marekani kwa Ghana.

Waziri wa mambo ya nje Antony Blinken amesema sera ya kizuizi cha Visa itatumika kwa watu maalum wanaohujumu demokrasia

Marekani leo Jumatatu ilitangaza sera ya kuzuia visa kwa watu binafsi ambao Washington inadai wanahusika kuhujumu demokrasia nchini Ghana, kabla ya uchaguzi wa rais na bunge mwezi Desemba katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

“Sera hii ya kizuizi cha visa itatumika tu kwa watu maalum ambao wanahujumu demokrasia na haiwahusishi moja kwa moja na watu wa Ghana wala serikali ya Ghana”, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amesema katika taarifa.