Marekani imebadilisha mfumo wa Viza kuingia Marekani

US Visa

Utaratibu mpya ulipendekezwa mwaka 2018 unatarajiwa kuathiri takribani watu milioni 15 ikiwemo watu wanaoomba kuingia Marekani pamoja na wale wenye matumaini ya kusoma, kufanya biashara, kazi au kuja tu kutembea

Takribani kila mtu anayeomba visa ya kuingia Marekani atatakiwa kutoa akaunti zao za mitandao ya kijamii pamoja na taarifa zingine binafsi kama sehemu ya utaratibu mkali wa utawala wa Trump wa kuhakiki wahamiaji na wageni wote.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inaeleza kwamba imefanya mabadiliko kwenye fomu za kuomba visa kwa wahamiaji na wasio wahamiaji zikimtaka muombaji kutoa taarifa za miaka mitano iliyopita za shughuli zao kwenye mtandao wa kijamii, nambari ya simu, barua pepe, safari za kimataifa na ikiwa amefukuzwa kutoka nchi hii. Pia wataulizwa iwapo mwanafamilia yeyote amehusika katika kazi za ugaidi.

Rais wa Marekani, Donald Trump

​Utaratibu mpya ulipendekezwa kwanza mwaka 2018 unatarajiwa kuathiri takribani watu milioni 15 ikiwemo watu wanaoomba kuingia Marekani pamoja na wale wenye matumaini ya kusoma, kufanya biashara, kazi au kuja tu kutembea. Waombaji wa kidiplomasia na visa rasmi pekee hazihusishwi na utaratibu huu mpya.

Awali taarifa binafsi juu ya kazi zilikuwa zikitakiwa kwa waombaji ambao wana weka kitisho cha usalama. Inakadiriwa waombaji takribani 65,000 kwa mwaka wanashindwa kwenye kipengele hicho.