Marco Rubia ameanza rasmi kazi kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio akizungumza baada ya kuapishwa mjini Washington, DC. January 21, 2025.

Rubio ameanza kazi akiwa mwenyeji wa mkutano na wenzake kutoka Australia, India na Japan.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio ameanza kazi rasmi leo Jumanne, akiwa mwenyeji wa mkutano na wenzake kutoka Australia, India na Japan siku moja baada ya rais Donald Trump kuanza muhula wake wa pili madarakani.

Mkutano wa kile kinachoitwa Quad, nchi nne zenye wasiwasi juu ya kuongezeka kwa nguvu ya China, utafanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na umeandaliwa kuashiria kuwa kukabiliana na Beijing ni kipaumbele cha juu kwa rais mpya.

Pia inaandaa jukwaa kwa viongozi wa nchi za Quad kufanya mkutano wa mapema katika urais wa Trump, mtu anayehusika katika kupanga mikutano hiyo alisema.