Marburg yaua watu 20 Equatorial Guinea

Muuza magazeti katika mji mkuu wa Uganda Kampala, Oktoba 6, 2014. Picha na Reuters.

Mlipuko wa virusi vya Marburg nchini Equatorial Guinea umesababisha vifo vya watu 20 katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, Shirika la Afya Duniani limesema Alhamisi.

Mlipuko wa homa ya kuvuja damu, ambayo inafanana na ugonjwa hatari wa Ebola, sasa umeenea na kuvuka jimbo la Kie-Ntem, ambako ulisababisha vifo vya kwanza kujulikana mwezi Januari. Ugonjwa huo wa virusi hivyo vya Marburg umefika Bata ambao ni mji mkuu wa kiuchumi wa nchi hiyo ndogo ya Afrika ya Kati, kwa mujibu wa taarifa ya serkali.

Kuenea kwa Marburg "ni ishara muhimu ya kuongeza juhudi za majiby ya haraka kupambana na kukomesha mlolongo wa maambukizi pamoja na kuepusha uwezekano wa mlipuko mkubwa na kupoteza maisha," alisema Dk Matshidiso Moeti mkurugenzi wa kanda wa WHO kwa Afrika.

Kati ya Machi 11-20, visa vinane vipya viligunduliwa, sita kati hivyo vilisababisha vifo, serikali ya Equatorial Guinea ilisema kwenye tovuti yake bila kutoa idadi ya kamili ya vifo tangu janga hilo lianze.

WHO imesema kuwa "hadi sasa, kuna uwezekano wa visa 20 na vifo 20" nchini humo.

Visa hivyo vipya vimeripotiwa kutoka katika maeneo ya Kie-Ntem upande wa mashariki na katika majimbo ya Litoral kwa upande wa magharibi na Centro Sur, ambayo yote yanapakana na nchi za Cameroon na Gabon.

Huko Afrika Mashariki, Tanzania ilisema Jumanne kuwa watu watano wamekufa kutokana na virusi hivyo, huku nchi jirani ya Uganda, ambayo ilikuwa na mlipuko wake wa mwisho wa mwaka 2017, ilisema inachukua "tahadhari kubwa"

Mpaka sasa ugonjwa huo hauna chanjo au dawa ya kuzuia virusi, lakini matibabu yanayotathiniwa na WHO inawezekana kuwa ni pamoja na bidhaa zanazotokana na damu, kinga na madawa, pamoja na utoaji chanjo mapema, WHO inasema.