Mapigano makali yaendelea Tigray, Ethiopia

Tigray, Ethiopia

Mapigano makali yanaendelea katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia, baada ya waziri mkuu kuanzisha oparesheni ya kijeshi kujibu kile ametaja kama mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa serikali hiyo.

Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka katika eneo hilo tangu mwezi Septemba, wakati Tigreay lilipoandaa uchaguzi licha ya kuwepo amri ya serikali kuu kutofanya hivyo.

Serikali ilisema matokeo ya uchaguzi huo hayatambuliwi kisheria, na pande zote zimeshutumiana hivi karibuni kwa kupanga mapigano ya kijeshi.

Ofisi ya waziri mkuu Abiy Ahmed, imedai kwamba wapiganaji wa kundi la Tigray – TPLF, walijaribu kuiba silaha kutoka kwa kambi ya kijeshi iliyo sehemu hiyo.

Eneo la Tigray lina asilimia 5 pekee ya jumla ya watu nchini Ethiopia ambao ni milionii 110, na ina utajiri mkubwa kuliko sehemu zingine kadhaa za nchi.