Baada ya taarifa hiyo, hisa za kampuni ya Novavax zimeongezeka kwa asilimia 1.3 hadi dola 70.89 baada ya dozi zake mbili kuwa chanjo ya nne ya Covid kuidhinishwa kutumiwa na watu wazima hapa Marekani.
Kituo cha Marekani cha kuzuia na kudhibiti magonjwa (CDC) kinatakiwa kupitisha matumzi ya chanjo hiyo kabla ya kuigawa kwa wanainchi.
Jopo la washauri wa CDC kuhusu chanjo linatarajiwa kukutana Jumanne ijayo, lakini ratiba ya mkutano huo bado haijatolewa.
Mapema wiki hii, serikali ya Marekani ilisema ilipata dozi milioni 3.2 za chanjo ya Novavax, ambazo inapanga kuzigawa mara tu kiwanda hicho kitakuwa kimekamilisha zoezi la kupima ubora wa chanjo hiyo katika wiki chache zijazo.
Zaidi ya theluthi mbili za Wamarekani wamekwisha pata chanjo kamili ya Moderna, Pfizer au Johnson& Johnson.
Maafisa wa afya wa Marekani wanatumai kwamba watu waliopinga kudungwa chanjo ya Pfizer na Moderna ambayo inatengenezwa kwa teknolojia ya kisasa iitwayo mRNA, badala yake watakubali kudungwa chanjo ya Novavax inayotengenezwa kwa protini.
Chanjo hiyo ambayo tayari iliidhinishwa barani Ulaya, inatengenezwa kwa teknolojia ambayo ilitumiwa kwa miongo kadhaa kupambana na magonjwa kama homa ya ini na mafua.