Mamilioni ya Wanigeria wakumbwa baa la njaa

Mfanya biashara akiwa nje ya soko lililofungwa na kikosi kazi cha kupambana na COVID-19 kwa kudharau masharti ya kujilinda na ugonjwa huo mjini Abuja, Nigeria, on Feb. 2, 2021.

Mamilioni ya Wanigeria ambao wakati mmoja walikuwa katika msimamo thabiti wa kifedha sasa wanahangaika kupata chakula kutokana na janga la corona.

Mamilioni ya Wanigeria ambao wakati mmoja walikuwa katika msimamo thabiti wa kifedha katika taifa lenye watu wengi zaidi barani Afrika na uchumi mkubwa sasa wanahangaika kujilisha wenyewe na familia zao kutokana na janga la corona.

Takriban asilimia 18 ya kaya nchini Nigeria zina walau mtu mzima mmoja ambaye hali kwa siku nzima kwa wakati mmoja, ukilinganisha na asilimia 6 kabla ya janga hilo, kulingana na Benki ya Dunia.

Mfumuko wa bei uko katika kiwango cha juu mno, na bei ya chakula inachangia karibu asilimia 70 ya kuongezeka.

Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa limeonya kuwa gharama za uingizaji chakula ulimwenguni zinatarajiwa kuongezeka kwa viwango vya juu mwaka huu, kwani bei inaongezeka kwa bidhaa zote za kilimo na kuongezeka kwa bei ya nishati kunaongeza gharama za uzalishaji na usafirishaji.