Mamilioni wajitokeza kupiga kura India

Mamilioni ya Wahindi wamejitokeza Jumamosi kwenye vituo vya kupigia kura katika awamu ya mwisho ya uchaguzi wa duruhaua mbali mbali  nchini humo ambapo Waziri Mkuu Narendra Modi anawania muhula wa tatu madarakani.

Upigaji kura ulifanyika katika majimbo ya uchaguzi 58 katika majimbo nane na maeneo ya shirikisho huku kukiwa na wimbi la joto kali ambalo limeshuhudiwa katika sehemu za kaskazini mwa India likipanda hadi nyuzi joto 45 katika wiki iliyopita.

Chama cha Bharatiya Janata cha Modi, au BJP, ambacho kinachuana na muungano wa upinzani wa Chama cha Congress na vyama vya kikanda, kinatarajiwa kushinda uchaguzi huo.

Miongoni mwa ushindani unaofuatiliwanykwa karibu zaidi ni viti saba vya ubunge katika mji mkuu, Delhi, ambapo BJP inakabiliwa na mapambano ya pamoja yaliyoanzishwa na Chama cha Aam Aadmi kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa Delhi, Arvind Kejriwal na Chama cha Congress.