Zaidi ya vifo 100 vimeripotiwa kwenye zaidi ya majimbo 6 kusini mashariki mwa Marekani kutokana na kimbunga hicho kilichoanzia kwenye kaunti ya Big Bend, Florida Alhamisi jioni kabla ya kuendelea kwenye majimbo ya Georgia na South na North Carolina.
Mshauri wa wizara ya Usalama wa ndani wa Marekani, Liz Sherwood Randall, alisema huko White House kuwa hadi watu 600 bado hawajulikani walipo ingawa idadi hiyo huenda ikapungua kadri timu za uokozi zinavyofika maeneo ya ndani.
Kwa mijibu wa mtandao wa habari wa Poweroutage.us. takriban nyumba na biashara milioni 2.1 zilikuwa hazina umeme Jumatatu. Jeshi la kitaifa pamoja na wafanyakazi wa dharura kutoka majimbo 19 wamepelekwa kwenye majimbo yalioathiriwa.