Mamia ya watoto wafariki katika vituo vya lishe nchini Somalia

Wakimbizi wanaorejea Somalia.

Mamia ya watoto tayari wamefariki  katika vituo vya lishe nchini Somalia, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) lilisema Jumanne, siku moja baada ya shirika hilo la kimataifa kuonya kwamba baadhi ya maeneo ya Somalia yatakumbwa na njaa katika miezi ijayo.

Kanda ya Pembe ya Afrika iko katika msimu wa tano mfululizo wa msimu mbaya wa mvua. Njaa iliyotokea mwaka 2011 nchini Somalia ilisababisha vifo vya zaidi ya watu robo milioni, wengi wao wakiwa watoto.

Takriban watoto 730 wameripotiwa kufariki katika vituo vya chakula na lishe nchini kote kati ya Januari na Julai mwaka huu lakini idadi hiyo inaweza kuongezeka zaidi kwani vifo vingi haviripotiwi," Mwakilishi wa UNICEF Somalia Wafaa Saeed aliuambia mkutano wa waandishi wa habari Geneva.

Vituo hivyo ni vya watoto walio na utapiamlo uliokithiri pamoja na matatizo mengine kama vile surua, kipindupindu au malaria na vinachukuliwa kuwa picha tu ya hali ilivyo kote nchini.