Mamia ya wanaharakati wa mazingira waliandamana siku ya Jumamosi katika mji wa Busan Korea Kusini kudai kuwa na ahadi kubwa zaidi za kimataifa za kupambana na taka za plastiki katika mazungumzo ya Umoja wa Mataifa mjini humo wiki ijayo.
Takriban watu elfu moja wakiwemo wa vikundi vya asili, vijana na wakusanya taka wasio rasmi walishiriki katika mkutano huo, mratibu huyo alisema, huku baadhi yao wakiwa wamebeba mabango yanayosema ondoa uzalishaji wa plastiki na punguza uzalishaji wa plastiki kwa haraka sasa.
Wanaharakati hao waliandamana kuzunguka Kituo cha Maonyesho na Mikutano cha Busan, ambapo kikao cha tano cha Kamati ya Majadiliano ya Kiserikali (INC-5) kitafanyika kuanzia Jumatatu kujadili makubaliano ya kisheria ya kimataifa kuhusu uchafuzi wa plastiki.