Jeshi la Mali limesema ‘Burkina Faso na Mali zinatuma ujumbe Niamey, na lengo ni kudhihirisha mshikamano wa nchi hizi mbili kwa wananchi ndugu zetu wa Niger.”
Ujumbe huo ulitarajiwa kuwasili Jumatatu nchini Niger, kulingana na wizara ya mambo ya nje ya Niger.
Viongozi wa mapinduzi Jumapili walikaidi muda wa kikomo uliowekwa na jumuia ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi(ECOWAS) kumrejesha madarakani Rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohamed Bazoum au wakabiliwe na hatua ya kijeshi.
Mali na Burkina Faso, ambako wanajeshi walichukua madaraka kwa nguvu mwaka 2020 na 2022, zilionya katika taarifa ya pamoja kwamba zitachukulia uingiliaji kati wa kijeshi nchini Niger kama tangazo la vita.