Mali haitatoa taarifa kuhusu wahamiaji wake

Wahamiaji kutoka Mali na Eritria wakiwa kwenye boti kwenye bahari ya Mediterranean.

Wahamiaji kutoka Mali na Eritria wakiwa kwenye boti kwenye bahari ya Mediterranean.

Serikali ya Mali imesema Jumatatu kuwa haitsaidia Umoja wa Ulaya kuwatambua au hata kuwarudisha wahamiaji wake nyumbani.

Serikali ya Mali imesema Jumatatu kuwa haitsaidia Umoja wa Ulaya kuwatambua au hata kuwarudisha nyumbani wa Mali walioko huko kinyume cha sheria. Mazungumzo yanaendelea kuhusu swala hilo wakati umoja wa Ulaya unapojaribu kukabiliana na uhamiaji haramu kupitia ushirikiano na mataifa wanakotoka.

Mbinu hiyo imetumika mapema mwezi huu wakati Niger ikipokea mamilioni ya dola ili kutoa ushirikiano na taarifa kuhusu wahamiaji wake. Waziri wa mambo ya nje wa Mali Abdoulaye Diop aliambia wanahabari Jumatatu mjini Bamako kuwa serikali yake inachoshugulikia kwa sasa ni usalama wa watu wa Mali walioko kwenye mataifa ya nje.

Umoja wa Ulaya unajadilia mkataba wa dola milioni 160 na Mali ili kufanikisha kurudishwa kwa wahamiaji nchini humo.