Wote wamelaumu ECOWAS kwa hatua kandamizi za kuwawekea vikwazo, kama njia ya kuwalazimisha kuachana na mapinduzi yaliofanyika kwenye mataifa yao. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, ECOWAS kupitia taarifa imesema kwamba haijafahamishwa rasmi kuhusu uamuzi wa mataifa hayo.
Viongozi wa kijeshi wa mataifa hayo kupitia taarifa ya pamoja iliyosomwa kupitia televisheni zao zote za kitaifa, wamesema kwamba,” wamemua kupitia utaifa wao kamilili kujiondoa mara moja kwa Burkina Faso, Mali na Niger kuondoka ECOWAS, “ wakidai kuwa shirika hilo limeondoka kwenye malengo ya waanzilishi wake pamoja na wanaharakati wa Umoja wa Afrika, baada ya kuwepo kwa karibu miaka 50 tangu kubuniwa.
Kando na hilo, wameongeza kwamba ECOWAS kupitia ushawishi wa mataifa ya kigeni, imeondoka kwenye misingi ya waanzilishi wake, na kuwa tishio kwa mataifa wanachama, pamoja na wananchi wao, kinyume na kuhakikisha furaha yao. Tutakuletea mengi Zaidi kuhusu taarifa hii, baadaye kwenye matangazo haya.