Waziri mkuu awafuta viongozi Malaysia.

Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak.

Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak ambae anaendelea kusongwa na tuhuma za ufisadai amemsimamisha kazi makamu wake pamoja na mkuu wa sheria. Kwenye taarifa alioitoa kwa njia ya televisheni Jumanne, Bw Najib ametangaza kuondolewa kwake naibu waziri mkuu Muhyiddin Yassin ambae amekuwa akimkosoa zaidi.

Hapo awali, taarifa kutoka kwa serikali ilisema kuwa mkuu wa sheria Abdul Gani Patail alisimamishwa kwa sababu za ki afya. Patail alikuwa amesaidia kwenye uchunguzi wa iwapo waziri mkuu alikuwa amepokea zaidi ya dola milioni 700 kutoka kwa hazina ya serikali ya 1MBD.

Madai hayo yalijitokeza mapema mwezi huu kwenye jarida la Wall Street lililotumia taarifa kutoka kwa stakabadhi za serikali za uchunguzi wa hazina ya serikali ya 1MBD. 1MBD hazina ambayo mwenyekiti wake ni Bw Najib, inakabiliwa na tuhuma za ufisadi, usimamizi mbaya na kusongwa na deni la zaidi ya dola bilioni 11. Hazina hiyo inachunguzwa na mashirika mengi ya serikali.