Taifa hilo la Kusini mwa Afrika limekuwa likikabiliana na mlipuko wake mbaya wa kipundupindu ambao haujawahi kutokea, huku zaidi ya watu 30,600 wakiambukizwa ugonjwa huo tangu visa vya kwanza viliporipotiwa mwaka jana.
Mwezi Novemba, Malawi ilipokea dozi milioni 3 za chanjo ya kipindupindu inayotolewa kwa njia ya mdomo kutoka Umoja wa mataifa kuanzisha kampeni lakini idadi ya maambukizi inazidi kuongezeka.
“Tumetumia chanjo zote tulizokuwa nazo,” msemaji wa wizara ya afya Adrian Chikumbe ameiambia AFP.
Idadi ya vifo ilifikia 1,002 Jumanne, na kuvuka idadi ya hapo awali ya mlipuko huo mkubwa, ambao uliua watu 968 kati ya 2001 na 2002, kulingana na shirika la afya duniani (WHO).