Kuongezwa muda kwa makubaliano hayo ni hatua inayojiri wakati makubaliano ya awali yalifikiwa chini ya usimamizi wa Uturuki na Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Julai, yakieleka kufikia muda wake wa mwisho.
Katibu mkuu wa Umoja wa mMtaifa Antonio Guterres amesema kwamba amefurahishwa na hatua hiyo, na kuongezea kwamba ataendelea kuhakikisha kwamba usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine unaendelea vyema.
Katika taarifa, Guterres ameongezea kwamba anaendelea kufanya kazi kuhakikisha kwamba vizuizi vyoye vinavyohusiana na usafirishaji wa chakula na mbolea kutoka Russia, vinaondolewa.
Makubaliano hayo yaliyosainiwa Istanbul, Uturuki, yanalenga kuhakikisha kwamba bei ya chakula na mbolea inashuka ili kuhakikisha kwamba hakuna uhaba wa chakula kote duniani.