Majirani hao wamekuwa na mzozo tangu Ethiopia isiyokuwa na bandari ilipofikia makubaliano mwezi januari na mkoa uliojitenga na Somalia wa Somaliland, kukodisha ukanda wa pwani kwa ajili ya bandari na kambi ya jeshi.
Kwa upande wake somaliland iliyojitangazia uhuru wake kutoka somalia mwaka 1991 katika hatua ambayo haitambuliwi na Mogadishu, ilisema Ethiopia itaitambua rasmi ingawa hili halijathibitishwa na Addis Ababa.
Somalia imesema makubaliano hayo ni ukiukwaji wa uhuru wake, na hivyo kuzusha tahadhari ya kimataifa kuhusu hatari ya kuzuka upya migogoro katika eneo hilo lenye hali tete.