Wizara ya ulinzi ya Russia ilidai siku ya Jumapili kwamba kulikuwa na mashambulizi zaidi ya Ukraine kwenye mtambo huo katika muda wa saa 24 zilizopita, siku moja tu baada ya Moscow na Kyiv kushutumiana kila upande ikilenga kiwanda kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya, jambo ambalo limezua wasiwasi mkubwa wa kimataifa.
Kampuni ya nyuklia ya Ukraine Energ-oatom ilisema haina taarifa mpya kuhusu mashambulizi kwenye kiwanda hicho.
Kiwanda hicho kilitekwa na wanajeshi wa Russia mwezi Machi, lakini bado kinaendeshwa na wafanyakazi wa Ukraine, eneo hilo la mstari wa mbele wa kusini wa vita limekuwa moja ya changamoto kuu za mzozo huo uliodumu kwa miezi sita.
Gavana wa mkoa Oleksandr Starukh alisema kwenye Telegram siku ya Jumapili kwamba vikosi vya Russia vilipiga majengo ya makazi katika mji mkuu wa mkoa wa Zaporizhzhia, karibu saa mbili kwa gari kutoka kwenya kiwanda hicho, na mji wa Orikhiv upande wa mashariki.