Makombora ya Hypersonic yanaweza kupunguza matatizo ya ulinzi; McCaul

Mfano wa kombora aina ya Hypersonic. March 1, 2018.

McCaul alisema utengenezaji wa makombora unaofanywa na Australia na Marekani unaweza pia kuongeza kizuizi kwa Indo-Pacific

Utengenezaji wa pamoja wa makombora ya hypersonic unaofanywa na Australia na Marekani unaweza kupunguza matatizo ya viwanda vya ulinzi wa Marekani na kuongeza kizuizi katika eneo la Indo-Pacific, mbunge wa Republican wa Marekani, Michael McCaul alisema akiwa Sydney leo Ijumaa.

Katika mahojiano, mwenyekiti wa kamati ya masuala ya mambo ya nje katika Baraza la Wawakilishi la Marekani amesema kuwa utengenezaji wa silaha za kisasa wa Australia unatoa mfano wa jinsi leseni iliyoratibiwa ya teknolojia ya ulinzi ya Marekani, pamoja na msamaha wa leseni kwa asilimia 70 ya mauzo ya nje kwa vifaa vya ulinzi kwenda Australia kuanzia Septemba Mosi itaisaidia Marekani kushindana na China katika kutengeneza silaha za kisasa.

Makombora ya Hypersonic, ambayo husafiri katika anga ya juu zaidi ya mara tano ya kasi kuliko mawimbi ya sauti, yalifanyiwa majaribio na China mwaka 2021, na kusababisha mashindano ya teknolojia na Marekani. Matumizi yake ya hivi karibuni yaliyofanywa na Russia katika vita vya Ukraine, yalizua wasiwasi miongoni mwa wanachama wa NATO.