Korea Kaskazini yafanya jaribio la makombora

Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un

Korea Kusini inasema makombora hayo yalirushwa leo asubuhi kutokea jimbo la kaskazini la Hwanghae.

Korea Kaskazini ilirusha makombora mawili ya masafa mafupi baharini, inayodaiwa kuwa ni kujibu majaribio ya kijeshi ya Korea Kusini na Marekani.

Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini inasema makombora hayo yalirushwa leo asubuhi kutokea jimbo la kaskazini la Hwanghae. Makombora hayo yaliruka kwa takriban kilomita 500 na kuangukia kwenye maji ya ufukwe wa mashariki wa nchi hiyo kwa mujibu wa maafisa wa Seoul.

Kurushwa kwa makombora hayo ni jambo la kawaida pale hali ya msuguano inapoongezeka katika penyusula ya Korea. Korea Kaskazini inachukizwa na mazoezi ya kijeshi yanayofanywa na Seoul na Washington na kuyaita maandalizi ya kuivamia Korea Kaskazini.