Makamu wa Rais Kamala Harris atafanya ziara ya wiki moja barani Afrika mwishoni mwa Machi huku Marekani ikiongeza mawasiliano yake kwa bara hilo huku kukiwa na ushindani wa kimataifa, haswa na China.
Safari hii itaimarisha ushirikiano wa Marekani kote barani Afrika na kuendeleza juhudi zetu za pamoja kuhusu usalama na ustawi wa kiuchumi, ilisema taarifa kutoka kwa msemaji wa makamu wa rais, Kirsten Allen ilieleza.
Mipango ya Harris inafuatia ziara za mke wa rais Jill Biden na waziri wa fedha Janet Yellen. Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken anaenda wiki hii, na Rais Joe Biden anatarajiwa kusafiri barani Afrika baadaye mwaka huu.
Hata hivyo, Harris ataangaliwa kwa karibu kama makamu wa kwanza wa rais mweusi katika historia ya Marekani na mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.
Anapanga kwenda Ghana kuanzia Machi 26 hadi 29, kisha Tanzania kuanzia Machi 29 hadi 31. Na kituo chake cha mwisho kitakuwa Zambia Machi 31 na Aprili mosi.