Makabiliano yametokea mapema leo Jumatano kati ya waandamanaji wanaounga mkono Palestina na wanaopinga maandamano hayo, katika chuo kikuu cha California, Los Angeles.
Wanaopinga maandamano hayo wanaripotiwa kurusha vitu kujaribu kuvunja vizuizi vilivyowekwa katika katika eneo hilo.
Katika mji wa New York, polisi wameidhinisha maandamano ya kuunga mkono Palestina katika chuo kikuu cha Columbia, ambako waandamanaji walilizingira jumba kuu la chuo hicho.
Maafisa wa chuo hicho wametangaza maandamano hayo kuwa kinyume cha sheria na yanayokiuka sera ya chuo.
Polisi walishika doria baada ya ombi la chuo lakini hawakufanikiwa kuwatenganisha waandamaji kwa haraka.
Darzeni ya waandamanaji wamekamatwa katika chuo kikuu cha Colombia, New York.