Majeshi ya Israeli yaipa "kichapo kikali" Syria, Iran

Mabaki ya ndege ya kivita F-16 ya jeshi la Israeli.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jumapili kuwa taifa lake limeyapa "kichapo kikali” majeshi ya Iran na Syria nchini Syria na kwamba wataendelea kukabiliana na mashambulizi mengine ya aina yoyote ile.

“Jana (Jumapili) tuliwapa "kichapo kikali" majeshi ya Iran na Syria. Na tuliweka bayana kwa kila mtu kwamba kanuni zetu za mapambano hazijabadilika kabisa. Tutaendelea kushambulia jaribio lolote la kutudhuru, hiyo imekuwa sera yetu na itaendelea kuwa sera yetu.”

Mashambulizi ya Jumamosi yamefanyika baada ya majeshi ya ulinzi ya Syria kuitungua ndege ya kivita ya Israeli aina ya F-16 kwa kombora lenye kushambulia ndege, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Israel ndege yake ya kivita kupigwa tangu vita ya mwaka 1982.

Marubani wa Israeli waliweza kutoka katika ndege hiyo, ambayo ilianguka ndani ya eneo la Israel, kwa mujibu wa Jeshi la Israeli. Israeli imesema kuwa mmoja wa marubani hao alijeruhiwa “vibaya sana” wakati wa “kuokolewa kwa dharura” na mwengine aliumia kidogo.

Maafisa kadhaa wa Israeli amesema wamekataa kukubali kuwepo majeshi ya Iran nchini Syria, jambo ambalo Tehran inakanusha kuwepo kwao.

Mashambulizi ya anga ya Israeli ni muhimu kuliko yote tangia vita ya wenyewe kwa wenyewe kuanza nchini Syria miaka saba iliopita.anzania