Majeshi ya Iraq yaanza mashambulizi mapya dhidi ya IS

Mosul, Iraq

Majeshi ya Iraq yameanza upya mashambulizi dhidi ya kundi la Islamic State siku ya Jumatano huko Mosul wakiwa na silaha kali kuelekea maeneo ya vijiijini.

Mashambulizi yalisimama kwa wiki kadhaa baada ya majeshi ya Iraq kukutana na upinzani mkali kutoka kwa kundi hilo.

Watu wanakimbia vijiji hivyo wanasema kundi la ISIS limejenga maahandaki ili kujificha usiku katika maeneo hayo na pia wanawalipua mabomu wa kujitoa muhanga ili kuwazuia majeshi ya Iraq.