Majaribio salama ya chanjo ya Ebola yanafanyiwa kazi haraka ili yaweze kuanza kufanyiwa binadamu katika muda wa wiki chache zijazo.
Kampuni ya madawa ya Uingereza GlaxoSmithKline ilisema Alhamis kuwa chanjo hiyo inatazamiwa kufanyiwa majaribio kwa watu wa kujitolea na ambao wako katika njema nchini Uingereza na Marekani katikati ya mwezi Septemba na kisha majaribio hayo kufanyiwa watu nchini Gambia na Mali.
GlaxoSmithKline inashirikiana na taasisi za kitaifa za afya za Marekani kutengeneza chanjo hiyo pamoja na shirika la afya lenye makao yake Uingereza, Wellcome Trust, ili kugharamia majaribio ya chanjo hiyo.