Majaji wa upelelezi wa Misri wamewafikisha kwenye mahakama ya uhalifu watu 43 ikiwa ni pamoja na raia 19 wa Marekani wanaoshutumiwa kwa kuhusika na shughuli zilzopigwa marufuku za makundi ya kidemokrasia ambayo yanapata kile Cairo ilichokiita pesa haramu kutoka nje.
Taarifa iliyotolewa jumapili na majaji wanaochunguza kesi hiyo iliorodhesha moja ya mashitaka kuwa ni kuendesha mashirika bila vibali vinavyotakiwa.
Msemaji wa wizara ya sheria amesema wale walioshitakiwa ni pamoja na Waserbia watano , wajerumani wawili , waarabu watatu na idadi ya wamisri wasiotajwa na miongoni mwa Wamarekani 19 ni Sam Lahood kiongozi wa ofisi ya Misri ya International Republikan Institute na mtoto wa waziri wa usafirishaji wa Marekani Ray La Hood.