Wito wa kuzuia waislam kuingia nchini Marekani ikiwa ni matokeo ya shambulizi liliopelekea mauaji ya watu wengi huko Orlando Florida kutokana na muuaji huyo kuapa kuonyesha kuunga mkono kundi la Islamic State unaweza kutia dosari katika mahusiano ya Marekani na washirika wake katika mataifa yaliyo na waislam wengi amesema afisa mmoja wa taasisi moja ya kiraia iliyo na waislam wengi hapa Marekani.
“Ukiwa na hali yeyote ambapo washirika wana wasi wasi kuhusu uwezekano wa tabia mbovu kama mtu akiingia White house , nafikiri hiyo inaweza kuharibu uhusiano wetu na dunia nzima alisema Ibrahim Hooper msemaji wa kitaifa katika baraza la mahusiano ya dini ya Kiislam Marekani.(CAIR).
Maneno hayo yalitolewa Jumatatu baada ya mgombea mtarajiwa wa chama cha Republikan Donald Trump kurudia wito wake wa kuwapiga marufuku kwa muda waislam kuingia Marekani kufuatia mauaji ya Jumapili kwenye klabu moja inayotumiwa sana na mashoga.
Mamlaka zinasema Omar Saddiqui Mateen, Mmarekani Muislamu ambaye wazazi wake ni wa Afghanistan, alitangaza utiifu wake kwa kundi la Islamic state na kiongozi wake Abubakr al Baghdadi wakati akifyatua risasi huko Orlando na kuuwa watu.